Mbonyo

Sunday 29 May 2016

Mheshimiwa sana Rais ndoto yangu ni kuona wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa na chaguzi za aina ya usafiri wanataka kutumia kwenda kazinin au katika shughuli zao binafsi. Ni wakati mwafaka sasa kwa majiji na miji yetu kuwa na uchaguzi wa aina ya usafiri wanaotaka kutumia. Wakitaka kutembea kwa miguu sawa, baisikeli sawa, bodaboda sawa, daladal swa na kadhalika. Tunalo tatizo kubwa la matumizi ya barabara na uzingatiaji wa sheria za usalama barabarani. Barabara zetu zimekuwa ni kwa matumizi ya vyombo vya moto huku sisi wapita kwa miguu na baiskeli tukiwa hatujui keshio yetu. Watati umefika sasa kwa miji yetu kuwa na njia za baiskeli na wapita kwa miguu. Hii inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa makali ya maisha huku tukifaidika na kuiweka miili yetu katika hali nzuri. Hivyo basi kipaumbele changu cha pili ni kutengenezwa kwa njia za watembea kwa miguu na baiskeli kama ilivyo nyumbani kwa wajomba.



Picha wakazi wa Montreal wakivinjari kuvuka mto wa mt. Laurence

No comments:

Post a Comment

Blog Archive