Mbonyo

Sunday, 29 May 2016

Mheshimiwa sana Rais ndoto yangu ni kuona wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa na chaguzi za aina ya usafiri wanataka kutumia kwenda kazinin au katika shughuli zao binafsi. Ni wakati mwafaka sasa kwa majiji na miji yetu kuwa na uchaguzi wa aina ya usafiri wanaotaka kutumia. Wakitaka kutembea kwa miguu sawa, baisikeli sawa, bodaboda sawa, daladal swa na kadhalika. Tunalo tatizo kubwa la matumizi ya barabara na uzingatiaji wa sheria za usalama barabarani. Barabara zetu zimekuwa ni kwa matumizi ya vyombo vya moto huku sisi wapita kwa miguu na baiskeli tukiwa hatujui keshio yetu. Watati umefika sasa kwa miji yetu kuwa na njia za baiskeli na wapita kwa miguu. Hii inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa makali ya maisha huku tukifaidika na kuiweka miili yetu katika hali nzuri. Hivyo basi kipaumbele changu cha pili ni kutengenezwa kwa njia za watembea kwa miguu na baiskeli kama ilivyo nyumbani kwa wajomba.Picha wakazi wa Montreal wakivinjari kuvuka mto wa mt. Laurence

Saturday, 12 December 2015

Kipaumbele changu

Your excellency (nimekosa maneno katika lugha yangu) ndugu Rais JP Maguguli nilijitahidi kukusikiliza wakati ukihutubia bunge la kwanza la mhura wako. Hakika ulikonga nyoyo za wengi pamoja na mimi mwenye moyo mgumu. Kuna mambo ambayo kwetu ni yakawaida, na pengine ndiyo sababu hatukukuambia kuwa ni kero wakati wa kampeni na ndiyo ni msingi wa vipaumbele vyangu. Leo nitanza na kipaumbele cha kwanza na ninaomba ufanyie kazi. Kipaumbele namba moja ni ajali za barabarani, ambazo zinagharimu maisha ya watanzania kila kukicha na kulitia taifa katika hasara kubwa. Ajali imekuwa ni jambo la kawaida katika maisha yetu na ndiyo maana hatukukuambia wakati wa kampeni. naomba utupia jicho.

Friday, 4 October 2013

Hii ndiyo shule yetu, shule ya msingi Ndirima, ipo takriba ni kilomita kumi toka Peramiho. Zamani tulikuwa hatuli chakula cha mchana shuleni, nyakati hizi hula. Maandalizi ya chakula hufanywa na wazazi. Watoto/wanafunzi hutakiwa kwenda na kuni shuleni. Pamoja na jitihada hizi mwamko wa elimu umeshuka sana, watoto hawatilii maanani mafunzo yao siyo kama enzi za akina Mlorera.

Blog Archive