"Mavi ya kale hayanuki"
Waraka maalum kwa askari wote wa Tanzania
Na Samson Mwigamba
MAKALA hii ilikuwa itoke Jumatano
ya wiki iliyopita lakini kwa sababu za kiufundi ikashindikana.
Imekuwa ni bahati nzuri kwamba inapotoka leo ijibu swali la askari polisi
dereva wa gari la maji ya kuwasha. Askari huyo alimweleza Mwalimu Mkuu wa watu
jinsi roho inavyomuuma pale anapowamwagia watanzania wenzake maji hayo ya
kuwasha wakati wakidai haki yao. Askari uliyeuliza na wenzako wote someni
makala hii kwa utulivu. Huu ni waraka maalum kwa askari wote wa
majeshi yote vikosi vyote Tanzania Bara na Visiwani. Kwa lugha ya wazi zaidi
nazungumza na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania, askari wa Jeshi la Kujenga
Taifa, askari wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), askari wa Jeshi la Magereza na wale wa Jeshi
la Wananchi (JWTZ). Kuwa mwanajeshi lolote kati ya hayo niliyoyataja si dhambi
na si kweli kwamba kuwa mwanajeshi kunakuondolea uwezo wa kufikiri na badala
yake ukawa unafikiriwa na watu wengine. Wala haimaanishi kuwa askari kuwa kama
robot ndio nidhamu bora kuliko zote duniani. La hasha! Mimi nilikataa utumwa
huo!
Mwaka 1999 nilihitimu elimu ya
cheti cha ufundi mchundo yaani Full Technician Certificate (FTC) katika
uhandisi wa Elektronik na Mawasiliano ya Anga yaani Electronics &
Telecommunications Engineering kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam
(DIT). Nikiwa bado sijapata kazi ya maana, mwezi Aprili mwaka 2000 niliona tangazo
la kazi ya Radio Technician katika Jeshi la Magereza. Nikatuma maombi na kuitwa
kwenye usairi uliofanyika chuo cha maofisa wa Jeshi la Magereza Ukonga Dar es
salaam mwezi Juni 2000. Wote tuliofaulu usairi tulipangiwa siku ya kuripoti
chuo cha Magereza Kiwira kule Tukuyu Mbeya.
Kufika kule nilishuhudia mambo ya
ajabu. Ingawa wao hufurahia na kusema eti wanakutoa uraiani na kuwa mwanajeshi
lakini baadhi ya matendo yanayofanyika wakati wa mafunzo ya jeshi ni ya
kuwapumbaza askari wetu ili baadaye wakiwa kazini, watawala wawatumie
watakavyo. Nilishindwa kuvumilia kauli mbiu ya wakufunzi wa jeshi pale
walipoelekeza kwamba chochote kruta (askari mpya mafunzoni) unachoambiwa lazima
uitikie “ndiyo afande”. Nilishindwa kuitikia kwa mfano pale mkufunzi mmoja mwenye
cheo cha koplo alipotutamkia mfululizo wa sentensi zifuatazo:
Mkufunzi: Nyinyi makruta mbona wote hamkuja na majembe?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Hamkuambiwa makao makuu ya jeshi kwamba lazima mje na
majembe?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Kwa hiyo kwa kuwa hamkuambiwa na nyinyi hamkuyabeba?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Wote ni wapumbavu
pamoja na mama zenu waliowazaa.
Makruta: Ndiyo afande!
Ni hayo pamoja na mambo mengine
ya kulazimishwa kwenda kwenye kile kinachoitwa disko, ambapo pamoja na uchovu
wa kutwa nzima wa kazi ngumu na nyingi bado ni lazima ukae hapo mpaka saa 4
usiku tena ukinyooshewa kidole tu na mwenzako lazima usimame na kuimbisha wimbo
tena kwa tabasamu, wimbo mmoja wapo ukisema “Magereza ninavyokupenda nitakunywa
sumu juu yako”, ndiyo yaliyonifanya nikakataa kazi ya jeshi baada ya wiki moja
tu ya mafunzo. Siku niliyokataa jeshi ilikuwa ni Jumatano asubuhi ambapo
sikwenda mchakamchaka na wakati wenzako wanatawanyika kufanya usafi wa nje
maeneo mbalimbali, mimi nilibeba begi langu na kuanza kuondoka chuoni majira ya
saa moja na nusu hivi asubuhi.
Nilikamatwa na mkufunzi mmoja wa
jeshi na kupelekwa pamoja na begi langu kwa Afisa Mafunzo wa Chuo. Aliponiuliza
sababu nilimtajia mbili, kwanza kwamba sifurahii mambo ya jeshi na kubwa zaidi
kwamba mimi ni msabato na nimeambiwa na wenzangu kwamba hapa hakuna kwenda
kusali siku zote za juma ni kazi. Kitu ambacho sitaweza maana sabato takatifu
lazima nipumzike! Bila kuuliza zaidi aliconclude kwa kuniambia kwamba,
“sijawahi kuona mtu anaacha kazi kwa ajili ya mambo ya dini. Ni dhahiri wewe
ulikuja kutupeleleza na hivyo kazi yako imeisha sasa unataka kurudi. Tutakuweka
rumande tena ile ya polisi kwa wiki mbili wakati tunafanya upelelezi juu yako”.
Askari aliyenileta alianza kunivuta ili kunipeleka rumande lakini nilikataa
huku nikiendelea kujieleza kwa afisa mafunzo ili ajue kwamba sikuwa na mpango
huo aliousema.
Baada ya kuelemewa na hoja zangu
alinipeleka kwa Makamu Mkuu wa Chuo ambaye yeye alitumia zaidi Biblia
kunihubiri kwamba nakaidi amri ya mamlaka wakati hakuna mamlaka isiyotoka kwa
Mungu. Jibu langu lilikuwa fupi na lenye msimamo mzito kwamba ikiwa mamlaka ya
wanadamu inafika mahali inanena tofauti na Mungu, Mtume Petro ametuandikia
kwamba katika hali ya namna hiyo, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko Mwanadamu”. Na
yeye alinishindwa akanipeleka kwa Mkuu wa Chuo na wao wote wakiwepo. Ushauri
waliokuwa wakimpa mkuu wa chuo ni kwamba mimi niwekwe rumande kwanza ili
wafanye upelelezi. Lakini sikuyumba katika msimamo wangu. Nilimweleza mkuu wa chuo kwamba mimi ni raia na si mpelelezi. Nilizirudia rudia sababu
zangu za kuacha jeshi tena kwa ujasiri mkubwa na kumhakikishia mkuu wa chuo
kwamba akipa hayo ninayoyataka niko tayari kubaki jeshini.
Hatimaye kauli ya mwisho ya mkuu
wa chuo ilikuwa ni hii: “Jeshi ni wito. Tunaweza kumlamisha huyu kijana kuwa
mwanajeshi lakini baadaye ikatuletea madhara makubwa sana”. Akamalizia kwa
kusemaa, chukueni maelezo yake kwa maandishi kisha arudishe vifaa vya jeshi na.
Wakati naondoka nilimsikia afisa mafunzo akitoa maelekezo kwa walio chini yake
kwamba mwanafunzi mwingine wa jeshi akija kuripoti na kwenye daftari akajaza
kwamba ni msabato, msimsajili kwanza mpaka aje kwangu! Sijui kama wasabato
wameendelea kupokelewa kwenye hicho chuo cha magereza lakini ninachotaka askari
wote wa majeshi yetu yote na vikosi vyote, ni kwamba askari unaweza kusimama
kwa miguu yako na kufikiri kwa akili yako mwenyewe!
Ndugu zangu askari, nchi imefika
mahali ambapo waingereza hupenda kupaita critical point. Ni mahali ambapo wananchi
wako tayari kwa mabdiliko na watawala wako tayari kwa mapambano ili kubaki madarakani.
Katika point hii askari wetu wanakuwa na nafasi kubwa ya aidha kuwezesha mabadiliko
hayo kutokea kwa wakati wanaoutaka wananchi tena kwa amani ama kuyachelewesha
(si kuyazuia) na kusababisha yatokee baadaye kidogo kuliko wananchi walivyotaka
tena baada ya kumwaga damu nyingi ya watanzania wasio na hatia! Napenda kurudia
kwamba hakuna jeshi lolote duniani hata kama tungekusanya majeshi yote ya dunia
hii na kuyaleta Tanzania hawataweza kuizuia nguvu ya umma pale inapokuwa
imeamua kufanya mabadiliko. Napenda tena kurudia kwamba si lazima askari mfanye
kile ambacho wakubwa wenu wanataka na kuwaamuru kufanya. Tunaweza kusimama
imara na kutetea haki za watanzania tukiwamo na sisi askari. Niliwahi kugoma kutii amri ya kukamatwa na
kuwekwa rumande.
Lakini pia mifano ni mingi na
nisingependa kuchukua mifano kutoka nchi za Ulaya kama Uingereza ambako tulishuhudia
wananchi wakiandamana mitaani na askari wao hawakuwahi hata kumpiga kofi tu
mwandamanaji hata mmoja. Walipohojiwa na vyombo vya habari walisema dhahiri
kwamba waandamanaji ni raia halali wenye
haki ya kufanya kile wanachokifanya kwa mujibu wfa katiba na sheria za nchi
yao. Katiba ya Tanzania na sheria za nchi hii zinatoa haki kama zile za Uingereza.
Tofauti ni utekelezaji wa matakwa hayo ya kikatiba na kisheria. Watawala wa
Uingereza wako tayari hata kung’oka
madarakani ili kutekeleza matakwa ya nguvu ya umma. Lakini wale wa Tanzania
wako tayari kung’oa uhai wa raia wengi wengi ili mradi k kuzuia nguvu ya umma
inayodai haki na wanfuhafanya
kwa sababu ya hofu ya kung’oka madarakani, jambo ambalo hawataki kabisa
kulisikia. Na wawapo
Ndugu zangu askari napenda
kuwaambia kwamba yote inayoonyeshwa na watawala wetu zaidi ya kuwategemea nyinyi. Wanaminya haki
zenu nyinyi wenyewe, haki za wazazi wenu, dada na ndugu zenu, marafiki zenu, jamaa zenu na majirani zenu.
Chukulia mfano rafiki zangu Mtaki na Edwin. Tumesoma wote shule ya msingi pale
Magu. Nilichaguliwa kujiunga na Mazengo sekondari, shule kubwa na ya muda mrefu ambayo sasa imegeuzwa kuwa chuo kikuu
bila mabadiliko ya majengo. Shule iliyokuwa na maabara nne kwa maana ya maabara
ya baiolojia, kemia, fizikia na jiografia.
Ilikuwa ni sekondari ya ufundi na hakuna karakana ambayo haikuwepo. Shu le
iliyokuwa na waalimu wa kutosha, vyumba vya kutosha vya madaasa na vya kulala
mabwenini. Katika bweni ambalo la Ujamaa kwa mfano nilikokuwa naishi mimi, kuna
vyumba kadhaa havikuwa na watu. Darasa la Form IVA ambalo nilikuwemo lilikuwa
na wanafunzi 21 tu darasani. Na mazingira mengine mengi ambayo sitaweza
kuyataja hapa ambayo yanafanya wanafunzi wa leo wa chuo kikuu cha Mt. John
wajiulize kama kweli ile ilikuwa ni shule ya lhamna maktaba wala vitabu vya
kutosha, na mengineyo mengi mnayoyafahmu. Nikafaulu kwa kiwango cha daraja la
juu lilfiloniwezesha kuendelea mpaka chuo kikuu na kupata kazi nzuri kwenye
umoja wa mataiifa. Rafvki zangu nakumbuka mlivyoamua kujiunga na jeshi la polisi si kwa sababu mlipenda kazi hiyo
ama kwamba mlikuwa na wito wa kuwa polisi kama mnavyodanganywa kwamba jeshi ni
wito. Nakumbuka mlijiunga huku mkilalamika kwamba mnalazimika kujiunga huko kwa
sababu kiwango chenu cha ufaulu hakiwapi fursa ya kazi bora zaidi ya hiyo.
Lakini mimi nawafahamu vizuri. Najua uwezo wenu wa darasani. Mliathiriwa na
mazingira ya hovyo ya shule mlizosoma.
Rafiki zangu nyinyi wote leo ni
wakuu wa vituo vikuu vya polisi vya wilaya katika wilaya za Mbozi na Igunga.
Leo hii mimi nimeacha kazi ya umoja wa mataifa kwa ajili ya kushiriki vema
katika mapambano ya kutafuta ukombozi wa taifa hili. Wadogo zenu na wadogo
zangu mnawajua wako katika juhudi za kutafuta maisha lakini ni magumu. Wengine
walikosa kabisa nafasi ya kujiunga hata na hiyo Magu Day. Wakaishia Bulima na
Kinango ambako hali ilikuwa mbaya zaidi. Wakafeli kabisa na leo wanahangaika
hapa na pale lakini watawala wanawawekea mazingira magumu mno ya kuendesha
maisha. Na sasa chukulia nao wametambua hali yao duni inasababishwa na watawala
walafi na walaghai. Wamejaribu kutumia njia za kidiplomasia kudai haki zao
wanakutana na u cha watu wanaitwa wak uu wa wilaya na mikoa. Wanaamua
kuandamana mnashiriki kuamrisha askari walio chini yenu kuwapiga na kuwaweka
rumande na hatimaye kuwafungulia kesi za kubumba!
Askari wetu igeni mfano wa askari
wa Misri! Pale wananchi walipoamua kuandamana kukomesha utawala wa kidhalimu wa
miaka 30 chini ya Hosni Mubarak, askari
waliwalinda badala ya kuwapiga. Walikataa kwa sababu hata wao walikuwa wakiumizwa
na Mubarak lakini zaidi ya hayo, waliokuwa wakiandamana walikuwa ni dada zao na
ndugu zao na marafiki zao.
Hivi sasa nchi iko njia panda.
Ugumu wa maisha umeongezeka mara nne na zaidi. Watawala hawalioni hilo wala
hawajishughulishi kurekebisha hali ya mambo hususan hali ya uchumi. Wako busy
na kujiandaa kwa uchaguzi wa 2015. Mawaziri wako busy na kampeni za kuteuliwa
kuwa wagombea wa urais kupitia chama tawala hapo 2015 na rais naye yuko busy
kuandaa mtu wake ambaye anadhani akimrithisha jumba jeupe la pale Magogoni
atasema mwacheni Ndugu Kikwete apumzike kwa amani. Taifa limeamua kuandika
katiba mpya, rais na serikali yake na chama chake wameamua kuuteka mchakato
ingawa . haikuwemo kwenye ilani yao ya uchaguzi ili tu waturudishie katiba ya
1977 na kuipa jina juu ya jalada KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA
MWAKA 2014.
Natambua juhudi zinazoendelea
hasa zikiongozwa na CHADEMA kujaribu kumkumbusha rais kwamba katiba iko juu
yake na katiba ni mali ya wananchi na yeye anaajiriwa kwa katiba hiyo na si
yeye kujiandalia katiba ili atawale kwa ulaini. Lakini juhudi za kidipromasia
zikishindikana hapo ndo itabidi haki ya watu idaiwe kwa maandamano na hapo
askari wote tuungane na kuwa kama Misri kwa kuwa katiba mpya ni kwa maslahi
yenu pia!
Jaribuni kutafakari!
No comments:
Post a Comment