Mbonyo

Saturday, 12 December 2015

Kipaumbele changu

Your excellency (nimekosa maneno katika lugha yangu) ndugu Rais JP Maguguli nilijitahidi kukusikiliza wakati ukihutubia bunge la kwanza la mhura wako. Hakika ulikonga nyoyo za wengi pamoja na mimi mwenye moyo mgumu. Kuna mambo ambayo kwetu ni yakawaida, na pengine ndiyo sababu hatukukuambia kuwa ni kero wakati wa kampeni na ndiyo ni msingi wa vipaumbele vyangu. Leo nitanza na kipaumbele cha kwanza na ninaomba ufanyie kazi. Kipaumbele namba moja ni ajali za barabarani, ambazo zinagharimu maisha ya watanzania kila kukicha na kulitia taifa katika hasara kubwa. Ajali imekuwa ni jambo la kawaida katika maisha yetu na ndiyo maana hatukukuambia wakati wa kampeni. naomba utupia jicho.

No comments:

Post a Comment

Blog Archive