Mbonyo

Friday, 4 February 2011

JE BADO TUNAIMBA KWA FURAHA?

TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE

1. Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuwaza wewe, niamkapo ni heri mama wee
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

2. Tanzania Tanzania, ninapokwenda safarini,
Kutazama maajabu, biashara nayo makazi,
Sitaweza kusahau mimi, mambo mema ya kwetu hakika
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

3. Tanzania Tanzania, watu wengi wanakusifu,
Siasa yako na desturi, ilituletea uhuru
Hatuwezi kusahau sisi, mambo mema ya kwetu hakika
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.
Tunawajibika kurejesha heshima ya Taifa letu!

2 comments:

  1. Haswaaaa! kwa furha zote kabisa. Ahsante sana kwa wimbo huu naupenda sana naweza hata kukuimbia nikiwa usingizini ila mmmhh sijui kama kuna furaha kweli?

    ReplyDelete
  2. Wimbo ni mzuri sana, nikiusikia ukiimbwa nakumbuka siku utoto wangu. Kwasasa naona watu tunapoteza mapenzi na nchi yetu kwa kuwa wabinafsi zaidi na matunda yanaonekana: uhujumu na ufisadi kila kona. Tanzania nchi yangu!

    ReplyDelete

Blog Archive