Mbonyo

Tuesday, 28 December 2010

MILANGALI

Picha ni kwa hisani ya Bw. MNK

Leo nimekumbuka sana embe hasa zile zenye mng'ao "milangali'. Unaweza kuwa na maembe luluki lakini kuridhika hapana, mpaka uwe umepata "mlangali". Wakati huo, miaka ya 1980 shamba la bibi lilikuwa ng'ambo ya mto Likwambi, Ndirima, ilipokuwa ngome ya Nkosi Zulu. Kwakweli kulikuwa na miembe mingi, kwa uchache bolibo, sikila? mapunda, dodo, maji, sindano n.k. Ushindani ulijaa kwenye embe sikila na dodo, kwani kwa maeneo yale zilikuwa ni adimu. Walionufaika ni watu kutoka Mdunduwalo na Maposeni. Karibuni tukumbuke.

2 comments:

  1. Hodi wakolo nyumba? nimefurahi sana kuja hapa kwani nimejikuta kama nipo mdunduwalo kwa Zulu nakula maembe. nimependa sana kazi nzuri. Endelea kutuhabarisha.

    ReplyDelete
  2. Asante dada kwa kututia moyo

    ReplyDelete

Blog Archive